LAYIII

Hatimaye yametimia kwa Arsenal kupata saini ya mlinda mlango Petr Cech kutoka Chelsea kwa kitita cha pauni milioni kumi.
Mlinda
mlango huyo wa kimataifa kutoka Jamhuri ya Czech, ambaye amecheza zaidi
ya mechi 400 katika misimu 11 akiwa na timu ya Chelsea, amejiunga na
Arsenal the Gunners kwa mkataba wa miaka minne.
Cech, mwenye umri
wa miaka 33, alicheza mechi saba tu msimu uliopita baada ya nafasi yake
kunyakuliwa na mlinda mlango kutoka Ubelgiji Thibaut Courtois.
Cech amesema alifikiri angestaafia Stamford Bridge, alakini ameongeza kusema: "Maisha daima hayawi vile unavyofikiria yakawa."
Ameandika:
"Msimu ulioopita wa kiangazi, mambo yalibadilika na nikaelewa kuwa
sikuwa mlinda mlango chaguo la kwanza, lakini nilifikiria haukuwa wakati
mzuri kwangu kuondoka.
"Wakati wa msimu huo, ilieleweka wazi kuwa
hali yangu isingebadilika na kama ninavyofahamu siko katika kazi yangu
ambapo nastahili kuwa- Niliamua kuondoka na kutafuta changamoto mpya."
Kocha
wa Arsenal, Arsene Wenger anasema: "Petr Cech ni mchezaji ambaye
nimemtamani kwa muda mrefu na nimefurahi sana ameamua kujiunga nasi."
Cech,
alijiunga na Chelsea akitokea klabu ya Rennes ya Ufaransa Julai 2004 na
kushinda makombe 13 akiwa na Chelsea - likiwemo kombe moja la klabu
bingwa na mataji manne ya ubingwa wa ligi kuu ya England.