RAIS wa serikali ya mapinduzi zanzibar kutupiliambali ada za mitiani ya sekondari katika shehehe za miaka 51 ya mapinduzi zilizo fanyika mjini zanzibar juz
WAKATI Watanzania wakihitimisha maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi
Zanzibar, wakazi wa Zanzibar wamejikuta wakiadhimisha sherehe hizo kwa
mtindo wa pekee baada ya kufutiwa malipo ya ada kwa shule za msingi na
sasa elimu hiyo inatolewa bure visiwani humo.
Kama hiyo haitoshi, pia katika kilele cha maadhimisho hayo,
ilibainishwa kuwa kuanzia sasa wazazi hawatochangia malipo ya ada ya
mitihani ya kidato cha nne na cha sita.
Habari hizo njema zilibainishwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein, ambaye alisisitiza kuwa uamuzi huo
unatokana na utekelezaji wa dhamira ya mapinduzi ya Zanzibar ya
kuwapatia wanafunzi wote elimu bure, kama ilivyoasisiwa na hayati Karume
na kutangazwa Septemba 23, mwaka 1964.
Wakati Dk Shein akitangaza unafuu huo katika elimu kwa wakazi wa
Zanzibar, tayari Rais Jakaya Kikwete, naye hivi karibuni alitangaza
rasmi kuwa serikali inaangalia uwezekano wa kufuta ada katika shule zake
za sekondari.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, lengo la kufuta ada hizo ni kusaidia
wanafunzi wengi ambao wanashindwa kuendelea na elimu hiyo, kutokana na
ukosefu wa fedha waweze kuendelea na masomo yao.