Wednesday, 20 July 2016

LOWASSA AZIDI KUITAMANI 2020 AWATAKA VIJANA WAJIPANGE ZAIDI MBIO ZA URAIS

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa amelitaka baraza la vijana la CHADEMA Taifa kutokukubali kugawanywa katika misingi ya kisiasa na badala yake wajikite katika kukiimarisha chama hicho katika ngazi ya chini hasa vijijini.

VIDEO: VILOJA NA MBWEMBWE ZA MSANII IDRISS SULTANI MSHINDI WA BIG BROTHER AFRIKA HIZI NDIO BAADHI YA VIDEO ZAKE ZA KUCHEKESHA

Aliye kuwa mshindi wa shindano la big brother africa linalo fanyika nchini africa kusini kila mwaka idriss sultan amekuwa akijizolea umaarufu kila kukicha kutokana na vituko anavyo vionyesha huko

VIDEO:WEMA ALIVYO IMBA WIMBO KUTOKA LEBAL YA DIAMOND PLATNUMZ KWA HISIA KALI SANA

Kama ulipitwa ikiwa ni siku chache ndani ya interview cloudsfms wakiwa na christian bella kabla ya black tie ema sepetu aliuimba wimbo

KIJUE ALICHOKISEMA MAGUFULI KUHUSU GARI YA RAISI KUKAMATWA

Wakati akizungumza na Maafisa wa Jeshi la polisi aliowapandisha vyeo vya Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema kipindi cha nyuma jeshi la polisi lilikuwa linaweka historia mbaya.

Kuna baadhi ya polisi waliowahi kuumizwa siku za nyuma kutokana na kusimamia sheria. Kuna magari au mabasi ya wakubwa ndani ya polisi ambayo ilikuwa ukiyakamata unapata msukosuko kikazi na kimaisha.

Rais akatolea mfano akisema kulikuwa na mabasi yanayoitwa Buffalo, Happy Nation au Happy Tanzania ambayo ukiyagusa lazima utaondolewa kwenye cheo ulichopo.

Rais akawaomba Makamishna kwenda kufanya kazi bila woga na wahakikishe pia hawawabughudhi Maaskari walio chini yao wakati wanatimiza majukumu yao ndani ya sheria na Kanuni za utumishi wao.
VIDEO MAGUFULI AKIZUNGUMZIA KUHUSU SUKARI KAMA ULIKOSA KUIONA
‘’Hata kama askari atakamata gari la IGP, RPC, Waziri au Rais, mwacheni atimize majukumu yake ili wahusika wa hayo magari wakajieleze wenyewe mbele ya sheria. Sheria ni msumeno’’. Rais alisema.

Rais aliendelea kusema, ‘’tunawanyima nguvu hawa Maaskari wa chini wanapotimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria halafu tunawaambia liachie hilo gari. Akishatoka pale yule aliyekuwa amekamatwa huanza kutamba kweli kweli huku askari akiwa amevunjika moyo na nguvu katika kusimamia sheria. Niwaombe sana, Vyeo vyetu tuweke pembeni na sheria tuziweke pembeni’’.

advertise here