Watu ambao muunganiko wao umeunganishwa kutokea mbinguni iwe marafiki,
wapenzi au wanandoa basi matokeo ya kile walichounganishiwa huwa na
msisimko na ladha ya kipekee. Kama ni ndoa huwa na furaha na mmiminiko
wa Baraka. Kama ni muziki basi huwa ni muziki ambao si rahisi ladha yake
kuisha.
Alikufa Kwa Ngoma, Hawajui, Sikiliza, Msiache Kuongea,ukisikiliza hizi
nyimbo pasi na shaka utakubaliana kuwa sio tu ni moja kati ya nyimbo
kali kuwahi kutokea kwenye muziki wetu ila ni moja kati ya nyimbo bora
kabisa za kushirikiana katika muziki wa Bongo Flava.