Friday, 25 November 2016

KAMPENI YA KUMNG’OA TRUMP YASHIKA KASI

BONYEZA PICHA HAPA KUONA VIDEO HAPO

Ndoto za Donald Trump aliyechaguliwa hivi karibuni kuwa Rais wa 45 wa Marekani huenda zikayeyuka baada ya wajumbe sita wa Democratic watakaopiga kura za majimbo kuanzisha kampeni maalumu ya kuwashawishi wajumbe wengine kutomwidhinisha Rais huyo mteule.

Wajumbe hao ambao majina yao yalitangazwa jana wanaamini kuwa iwapo watafanikiwa kuwashawishi wenzao wengine 37 kutoka Chama cha Republican basi watakuwa wamefanikiwa

OMMY DIMPOZ: KUMBE KISA WEMA SEPETU OMMY DIMPOZ WALIVULUGANA NA DIAMONDPLATNUMZ

STAA wa Bongo fleva hapa nchini, Ommy Dimpoz anayetamba na ngoma yake ya ‘Kajiandae’, amefungukia bifu lake na msanii mwenzake, Diamond Platinumz kuwa chanzo cha ugomvi wao ni Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu ‘Madam’.

Akizungumza leo Novemba 24, 206 wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, Dimpoz amesema mwanzoni walikuwa na urafiki mzuri na Diamond na walikuwa wakishirikiana mambo mengi kuhusu muziki wao, lakini baadaye hali ilikuwa tofauti baada, Diamond akaanza kumpoteza na kukwepa kufanya naye baadhi ya mambo kwa pamoja.

Dimpoz amesema hayo baada ya Diamond kusema mambo kadhaa kuhusu yeye wakati akifanya mahojiano jana kwenye kipindi hicho cha XXL.

MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI MKUBWA WA KIHISTORIA WA KUHAMISHA MISULI

Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili jana kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji kwa kutumia darubini (microvascular surgery) wa kuhamisha misuli na mishipa ya damu kutoka kwenye mguu kwenda sehemu nyingine chini ya mguu (free gracilis muscle transfer).

Upasuaji huu wa aina yake na ambao mara nyingi huchukua muda wa saa sita hadi saba una lengo la kujenga uwezo kwa watalaamu wa ndani ili waendelee kutoa huduma za ubingwa wa hali ya juu kwa Watanzania wengi zaidi na vilevile kupunguza kasi ya kupeleka wagonjwa nje.

advertise here