Monday, 20 March 2017
KUHUSU NAPE KUJIUZURU
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesema endapo atashindwa kusimamia uhuru wa habari na vyombo vya habari nchini atakuwa hafai kubaki kwenye nafasi hiyo kwa kuwa atakuwa ameshindwa majukumu yake katika nchi huru
Nape ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia na kulaani kitendo kinachodaiwa kufanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, cha kuvamia chombo cha habari cha Clouds, akiwa na askari wenye silaha na kukifananisha kitendo hicho na kuinajisi taaluma ya habari.
Subscribe to:
Posts (Atom)