Sunday, 15 May 2016

NI MIEZI 6 SASA NIKO KWENYE MAHUSIANO NA GADNER

LIKE PAGE ETU HAPA FACEBOOK HUTAPITWA NA STORY YOYOTE


MUUZA sura kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Giggy Money’ amefunguka kuwa mtangazaji maarufu Bongo wa Clouds FM, Gardner G. Habash hachomoki kwake na hadi sasa wako kwenye uhusiano wa mapenzi kwa muda wa miezi sita.

Gigy mefunguka haya baada ya picha zinazomuonesha akiwa kwenye mapozi ya kimahaba na Gardner kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Giggy alisema mtangazaji huyo amekuwa mtu wa muhimu kwake kwa sasa.

“Kwani kuna tatizo nikiwa na Gardner? Yule ni mtu muelewa na sahihi kwangu, ninafikiri kupitia yeye nitajifunza mambo mengi na kuzidi kufanikiwa kwa sababu yeye ni moja kati ya watu ambao wako kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu,” alisema Giggy Money.

WANAOVAA SURUALI CHINI YA MAKALIO VIBOKO SABINI

LIKE PAGE YETU HAPA USIPITWE NA STORY TENA FACEBOOK
Boneza picha subscribe nasi utube upate habari kwa njia ya video
https://www.youtube.com/watch?v=mTFQTl-J334\
Wakazi wa Kata ya Karansi, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wametoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70.

  https://www.youtube.com/watch?v=mTFQTl-J334Uamuzi huo umefikiwa na wakazi zaidi ya 200 wakisema uvaaji huo ni kinyume na mila na desturi za Kiafrika.


Vazi lingine lisilotakiwa kwa wanawake ni kuvaa suruali pamoja na vijana kunyoa ndevu mitindo isiyofaa.


Mkutano huo ulioandaliwa na wazee wa kimila jamii ya Meru (Wachili) na Wamasai (Malaigwani), uliwavutia wananchi wengi ambao walihudhuria.


Sambamba na uamuzi huo utakaokuwa unafanyika hadharani, pia adhabu hiyo itawahusu wezi wa mali na wanaopenda kucheza pool table wakati wa kazi.


Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Wilbrod Mutafungwa alipinga uamuzi huo akisema kwa maazimio hayo ya kuwaadhibu watuhumiwa kwa kuwachapa viboko ni kujichukulia sheria mkononi na ni kinyume na sheria.

video ya mkenya aliyedandia helkopter

advertise here