Wednesday 15 February 2017

AUDIO: UMEIPATA HII YA BARNABA KUMFUMANIA MKEWE ISKIE HAPA



Mke wa Barnaba Akiwa na Bwana Mwigine 
Jana February 15 2017 kupitia XXL ya clouds FM, Soudy Bwown ametuletea U Heard inayohusu mwimbaji staa wa Bongofleva Barnaba kudaiwa kuachana na mke wake.

MANENO YA KIKWETE KUHUSIANA NA SWALA LA MADAWA YA KULEVYA



Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete, amefunguka kuhusu sakata la dawa za kulevya na kuipongeza serikali hususani Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuanzisha vita hiyo na kutaka wahusika wachukuliwe hatua.

Kikwete amefunguka hayo leo katika kipindi cha East Africa Breakfast cha EA Radio, kinachoruka kila siku saa 11:00 alfajiri hadi saa 3:00 asubuhi.

DIVA AFUNGUKA KUHUSU KUTAMANI KUDATE NA ALIKIBA

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Diva The Bosslady amefunguka kwa kudai kuwa katika mastaa wa muziki Alikiba ndiye msanii ambaye anatamani kudate naye.
Diva ambaye kwa sasa anatoka kimapenzi na muimbaji Heri Muziki, alikuwa host wa show ya Valentine’s Day iliyofanyika Jumatano hii katika ukumbi wa Next Door na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali.
Akiongea na waandishi kabla ya kwenda kusherehesha show hiyo iliyoandaliwa na Irene Uwoya, Diva alidai Alikiba ndiye msanii ambaye anatamani kudate naye.

BREAKING NEWS: MASOGANGE NDANI KWA SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA

TAARIFA zilizotufikia, zinaeleza kwamba video queen maarufu Bongo, anayefahamika kutokana na shepu yake matata, Agness Gerald almaarufu Masogange, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu (Central) akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.
Masogange alikamatwa na polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba, mpaka muda huu bado anashikiliwa central. Mwanadada huyo anaingia kwenye orodha ya wasanii wengine na watu maarufu Bongo,

HAKIMU NA KARANI KIZIMBANI KWA RUSHWA

https://www.youtube.com/watch?v=at4JVl5SZ38
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)  mkoani Mara imewapandisha kizimbani Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo mjini Musoma, Swalala Mathayo (40) na karani wa Mahakama hiyo, Charles Masatu (56) kwa tuhuma za kudai na kupokea rushwa.
Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Musoma, Richard Maganga, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Marshal Mseja, alidai  watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa  kuomba na kupokea rushwa ya

advertise here