Wednesday 15 February 2017

BREAKING NEWS: MASOGANGE NDANI KWA SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA

TAARIFA zilizotufikia, zinaeleza kwamba video queen maarufu Bongo, anayefahamika kutokana na shepu yake matata, Agness Gerald almaarufu Masogange, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu (Central) akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.
Masogange alikamatwa na polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba, mpaka muda huu bado anashikiliwa central. Mwanadada huyo anaingia kwenye orodha ya wasanii wengine na watu maarufu Bongo,
walioshikiliwa na wanaoendelea kushikiliwa wakihusishhwa na ishu ya matumizi na biashara ya madawa ya kulevya, katika vita kali inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Taarifa zaidi kuhusu kukamatwa kwa Masogange na kinachoendelea, zitaendelea kukujia kupitia hapahapa, endelea kufuatilia mtandao huu na pia kufuatilia SWAXBZ Blog

No comments:

Post a Comment

advertise here