Wednesday, 15 February 2017

HAKIMU NA KARANI KIZIMBANI KWA RUSHWA

https://www.youtube.com/watch?v=at4JVl5SZ38
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)  mkoani Mara imewapandisha kizimbani Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo mjini Musoma, Swalala Mathayo (40) na karani wa Mahakama hiyo, Charles Masatu (56) kwa tuhuma za kudai na kupokea rushwa.
Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Musoma, Richard Maganga, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Marshal Mseja, alidai  watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa  kuomba na kupokea rushwa ya
Sh 200,000.

Alidai   Hakimu Mathayo anatuhumiwa kwa makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa,wakati karani Masatu anatuhumiwa kushiriki katika kuiomba rushwa hiyo.

Mseja  alidai chanzo cha madai hayo ya rushwa ni kuwa hakimu huyo alitoa hukumu ya kifungo cha miaka miwili  kwa Magdalena Aloyce (29) mkazi wa mtaa wa Makongora mjini Musoma.

Alidai kwa vile mtuhumiwa alifungwa   akiwa na mtoto mdogo   wa miezi 10 na kuwaacha  wengine wawli bila  uangalizi, ndugu zake walimfuata mkuu wa gereza na kuomba mfungwa huyo apewa kifungo cha nje   aweze kuhudumia familiya yake ambayo inamtegemea.

Ndugu walipewa maelekezo  na mkuu wa magereza kwenda kwa ofisa wa ustawi wa jamii na walipofika walihudumiwa na kujaziwa fomu namba 12 kwa mujibu wa Sheria ya Kutumikia Jamii,  alisema.
Alisema  fomu hiyo ilitakiwa kuidhinishwa na hakimu aliyetoa hukumu hiyo.

Mseja alidai hakimu huyo hakuweza kufanya hivyo bali alitengeneza mianya ya kudai rushwa kwa kumuhusisha karani wake na hapo ndipo ndugu hao walipotoa taarifa Takukuru na kuwekwa mtego na hatimaye kukamatwa na rushwa hiyo ya Sh 200,000.
Watuhumiwa hao  walikana  mashitaka na wapo nje kwa dhamana hadi   Machi 21 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Na Shomari Binda-Mtanzania Mara

No comments:

Post a Comment

advertise here