Mawaziri wa utafiti kutoka bara
Ulaya wanaokutana mjini Lucerne, Uswizi wamesisitiza kwamba mpango wa
kutuma chombo maalum kinachoweza kusafiri kwenye sayari ya Mars mwaka
2021 bado utaendelea.
Wameahidi kutoa jumla ya euro €436m ambazo zinahitajika kufanikisha mpango huo.Mradi huo umechelewa kiasi na unagharimu pesa zaidi kuliko ilivyotarajiwa, jambo lililoibua wasiwasi kwamba mataifa wanachama wa Shirika la Anga za Juu la Ulaya (ESA) huenda wakaufuta