Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametoa onyo kali kwa mtu yeyote atakae kwamisha Kamati maalumu aliyoiunda ya kuchunguza kiwango cha madini yaliyomo kwenye mchanga uliowekwa kwenye makontena.
Amesema kuwa ameamua kuunda kamati hiyo yenye wasomi waliobobea katika masuala ya jiolojia, kemikali na uchambuzi wa kisayansi ili wawakilishe Watanzania zaidi ya milioni hamsini ambao wanataka kujua ukweli kuhusu rasilimali yao ya madini.