Jeshi la Polisi limekwama kuwafikisha mahakamani viongozi wanne wa Taifa wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), baada ya kukosea hati ya mashtaka.
Wanaoshikiliwa ni Mwenyekiti wa Taifa, Patrobas Katambi, Katibu Mkuu, Julius Mwita, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Joseph Kasambala na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya, George Tito.
Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema makosa