Hatimaye rapper Roma amesimulia mkasa wa kutekwa akiwa na wenzake watatu kuanzia Jumatano iliyopita hadi Ijumaa. Tumekuandikia kile alichosimulia.
Wakati naendelea na shughuli zangu, walifika watu ambao sikuweza kuwafahamu mbaya zaidi walikuwa na silaha za moto na amri yao ya kwanza ilikuwa ni ingia ndani ya gari. Baada ya kuingia tu ndani ya gari, nakumbuka wale watu walitufunga usoni na vitambaa na kutuamuru tuiname chini kwa order ya kwamba inama chini na usiinuke na wakiwa wameshika silaha za moto. Hofu yetu ikatufanya