Tuesday 10 May 2016

WANASAYANSI WAUNDA NGOZI YA KUTOA UZEE

FACEBOOK

Wanasayansi wanadai kuunda aina ya ngozi inayoweza kubandikwa juu ya mwili wa mtu kupunguza muonekano wa mikunjo ya ngozi mwilini na ngozi inayopwaya chini ya macho kutokana na uzee.
Ni aina ya maji maji mtu anayopaka mwilini alafu inaachwa kukauka ambapo baadaye husihia kuwa ngozi nyembamba iliyo mithili ya 'ngozi ya ujana, Nature Materials inaarifu baada ya kufanya majiribio kadhaa madogo.
Kwa sasa inafanyiwa majaribio ya kuuzwa kama bidhaa ya urembo.
Lakini wanasayansi Marekani wanasema "ngozi ya pili " huenda baadaye ikaweza kutumika kutengeneza dawa na kinga dhdi ya jua.
Ngozi ya pili

KIPA WA CAMEROON AAGA DUNIA

FACEBOOK

Kipa wa timu ya taifa ya Cameroon upande wa wanawake ameaga dunia baada ya kuzirai wakati wa mazoezi, Shirikisho la soka la Cameroon limesema.Jeanine Christelle Djomnang,mwenye umri wa miaka 26, aliuguwa kabla ya mechi ya Femina Stars Ebolowa kusini mwa Cameroon Jumapili na alifariki akipelekwa hospitalini.
Shirikisho hilo linasema taarifa za awali zinaashiria alikufa kutokanana mshtuko wa moyo lakini sasa linasubiri taarifa rasmi ya madaktari.

POLICE WAANDAMANA DHIDI YA BEYONCE

FACEBOOK

Kundi moja la maafisa wa polisi limefanya maandamano karibu na tamasha lililofanyika katika mji wa nyumbani wa nyota wa muziki Beyonce huko Houston.
Wanachama wa muungano wa polisi na Sherrif walisimama mbali na uwanja wa soka na kuelekeza mwangaza wa bluu katika ukumbi wa tamasha hilo.
Walikuwa wanapinga kanda ya video ya Beyonce ambayo wanasema inawaponza polisi.

UHABA WA SUKARI CHANZO MWESHIMIWA RAIS

FACEBOOK

Akihojiwa na Mtangazaji Yvonne Kamuntu kwenye Azam News, Mchumi mbobezi hapa nchini Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema uhaba wa sukari uliopo kwa sasa nchini umesababishwa na Rais John Magufuli mwenyewe kwa kuzuia sukari ya nje kutoingizwa Nchini, ilhali viwanda vyetu havikidhi idadi inayohitajika katika uzalishaji wake.

advertise here