Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku ameendeleza ‘vita’ yake
dhidi ya Paul Makonda, akisema yupo tayari kusaidia vyombo vya dola
kukamata vigogo wa dawa za kulevya na kuhoji ukimya wa mawaziri watatu
dhidi ya kile alichodai utajiri wa mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Awali, Kasheku ambaye ni maarufu kwa jina la Msukuma, alitoa tuhuma
dhidi ya Makonda juzi, alipotaka kujua wafadhili wa safari za mkuu huyo
wa mkoa nje ya nchi na sababu za kubagua watuhumiwa wa biashara ya dawa
za kulevya kwa kutaja baadhi na kuwaacha wengine, huku mawaziri wakisita
kuchukua