Watuhumiwa wa biashara na matumizi ya dawa za kulevya waliotajwa hivi
karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaamm, Paul Makonda, Jumanne hii,
February 7, 2017 wamefikishwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es
Salaam kujibu tuhuma zinazowakabili.
Mastaa hao wakiwemo TID, Nyandu Tozi, Babu wa Kitaa, Romy Jones, Tunda,
na wengine, wameachiwa kwa sharti la dhamana ya shilingi milioni 10 kila
mmoja na watakuwa wakiripoti kwa mwezi mara mbili huku
wakiwa katika uangalizi wa jeshi la polisi kwa kipindi cha mwaka mmoja.
wakiwa katika uangalizi wa jeshi la polisi kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Hata hivyo watuhumiwa wengine wakiwemo Petit Man, Said Alteza, Lulu Diva
na wengine wametakiwa kuweka dhamana ya shilingi milioni 20 na watakuwa
chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka mitatu. Iwapo watuhumiwa hao
watashindwa kufuata masharti hayo watarudishwa tena mahakamani.
Hali imekuwa tofauti kwa Wema Sepetu ambaye ameendelea kukaa rumande
baada ya msako kubaini msokoto wa bangi nyumbani kwake na hivyo
kuongezwa kosa jingine zaidi ya lile la awali, ambapo sasa inasubiriwa
uchunguzi kukamilika.
No comments:
Post a Comment