Wednesday 4 May 2016

MTANGAZAJI WA CLOUDSFM DIVA KASEMA NYIMBO ZAKE ZINABANIWA KUPIGWA REDIONI

SWAXBZ

Mtangazaji wa Clouds FM, Diva amesema nyimbo zake pamoja na za mtangazaji mwenzake, Adam Mchomvu zinabaniwa na redio zingine, kitu ambacho anaona si sawa.

Anasema redio za mikoani ndizo zimekuwa zikiwapa support bila kujali kuwa wanatoka Clouds lakini redio karibu zote za Dar zimekuwa zikibania nyimbo zao.

Diva ambaye anaandaa album yake, The Life of The Diva, amesema kuwa hicho ni kitu ambacho angependa kuona kinafutika.


“Mimi naona wako so unprofessional, mbona sisi Clouds FM watu wazuri, mimi Sam Misago kaja, katoa wimbo ataitwa kwenye XXL nyimbo yake itachezwa, sisi mbona nyimbo zetu hamchezi?” amehoji Diva.

“Nilipeleka nyimbo East Africa Radio na ina haki zote za kuchezwa na haikuchezwa kwasababu natoka Clouds Media, kwanini wanatufanyia hivi? Hii ni biashara, wao wafanye kazi zao, na sisi tufanye kazi zetu lakini when it comes to music, sisi tunafanya serious kabisa,” amesisitiza.

Chanzo: Bongo 5
Ulipitwa na clip hii ya adamore icheki hapa mtu wangu

No comments:

Post a Comment

advertise here