LAYIII
Hatimaye baraza kuu la Chadema
limeridhia kusimama kwa muda kufanya kazi za chama aliyekuwa katibu mkuu
wa chama hicho Dr Wilbrod Slaa.
Ni kishindo cha baraka za baraza
kuu la Chadema likiridhia kupumzika kwa Dk Wilibroad Slaa ambaye tangu
kujiunga kwa wazir mkuu mstaafu Edward Lowassa amekuwa haonekani katika
vikao vyetu vya chama hicho, katika ufunguzi wa mkutano wa baraza kuu la
Chadema mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe amekiri kuwa
licha ya Dkt Slaa kushiriki vikao mbalimbali vya chama kuhusu ujio wa
lowassa, lakini ni kweli alitofautian kimtizamo na wajumbe wa kamati
kuu.
Aidha Freeman Mbowe amekiri pia
juu ya hofu iliyokwisha kutanda kwa viongozi, wanachama na wapenzi wa
chama hicho juu ya ujio wa baadhi ya vigogo kutoka ndani ya chama cha
mapinduzi CCM.
Kwa upande wake kaimu katibu mkuu
wa Chadema taifa Salum Mwalimu akizungumza katika mkutano huo pamoja na
masuala mengine amewataka wanachama na wapenzi wa chama hicho
kuahkikisha wanaunganisha nguvu hasa katika kipindi cha uchaguzi.
Miongoni
mwa agenda kuu zilizojadiliwa katika baraza kuu la Chadema ni pamoja na
agenda ya kupitisha ilani ya chama hicho, kupendekeza majina ya
wagombea nafasi ya urais ikiwa ni pamoja na kuthibitisha mikakati na
rasilimali za kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu.
thank you for your help you real awasome
ReplyDeleteSend me your news using mswaxkim6@gmail.com
ReplyDelete