WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewatangazia kiama watu wote waliohusika kuwaua askari polisi nane Kibiti wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari hao jijini Dar es Salaam jana asubuhi Mwigulu alisema watu hao watakamatwa wote na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
"Kitendo hiki cha mauaji kilichofanyika dhidi ya askari wetu hakivumiliki hata kidogo waliohusika tutawatafuta na kuwakamata"alisema Mwigulu.