Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Japan umethibitisha kwamba kukaa kwa mda mrefu na kutazama vipindi vya televisheni kwa masaa mengi kunahatarisha afya kwani huhusishwa na maradhi yanasababisha mzunguko wa damu mwilini kutokuwa sawa.
Watafiti hao wanasema, hali hiyo pia huenda ikasababisha damu kuganda na kutengeneza vidonge katika sehemu kama vile miguu, na iwapo mgando huo utasukumwa na nguvu za mzunguko wa damu na kuingia sehemu kama vile mapafu, husababisha vifo.Utafiti huo ulihusiha watu zaidi ya 86,000 ambao hupendelea kutazama televisheni katika mida mbalimbali kwa siku.
Kisha afya zao zilifuatiliwa kwa zaidi ya miaka 19 tangu mwaka 1988 hadi 1990.