Wednesday, 8 February 2017
USHAIDI DHIDI YA KESI YA SCOPIONI MAPYA YAIBUKA DAKTARI AIBUA USHAIDI MZITO
Shahidi wa nne katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njwete, ameieleza Mahakama kuwa mtu aliyehusika kumtoa macho Said Mrisho alikuwa ni mzoefu wa vitendo hivyo na siyo wa kawaida.
Shahidi huyo, Dk Christine Mataka (52) ambaye ni daktari bingwa wa macho kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alitoa maelezo hayo katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala alipotoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa Njwete (34) katika kesi iliyopata umaarufu wa ‘kesi ya Scorpion’ kutokana na maelezo kwamba aliyefanya uhalifu huo ni Scorpion.
KUTAJWA KWA MBOWE DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA BUNGE LIMENUKA
Hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaja Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapo kesho kuhojiwa, imewachefua baadhi ya wabunge.
Wabunge waliohojiwa mjini Dodoma jana, walisema kinachoendelea ni siasa badala ya uhalisia.
Mbunge wa Kigoma Mjini, (ACT – Wazalendo), Zitto Kabwe alisema kinachoendelea ni siasa za kuchafuana na kwamba Makonda ajiandae kubeba msalaba wake katika jambo hilo.
VIDEO MAJIBU YA YUSUPH MANJI BAADA YA KUHUSISHWA NA MADAWA YA KULEVYA
Mfanyabiashara Yusufu Manji amesema kuwa atakwenda Kituo cha Polisi
kesho kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivyotaka.
Manji amesema kuwa pamoja na kuwa Makonda ametaka wafike Ijumaa yeye atakwenda kesho huku akihoji kuwa inawezekanaje wakaitwa watu 65 kuhojiwa kama hakuna shughuli za kufanya kwa siku nzima.
“Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa. Huwezi kunitangaza kupitia radio
Manji amesema kuwa pamoja na kuwa Makonda ametaka wafike Ijumaa yeye atakwenda kesho huku akihoji kuwa inawezekanaje wakaitwa watu 65 kuhojiwa kama hakuna shughuli za kufanya kwa siku nzima.
“Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa. Huwezi kunitangaza kupitia radio
VIDEO: ASKOFU GWAJIMA AJIBU MAPIGO KWA PAUL MAKONDA
Saa chache baada ya kutakiwa kufika polisi na mkuu wa mkoa kwa kutoa
taarifa juu ya madawa ya kulevya,Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na
Uzima,Josephat Gwajima Amepost Ujumbe picha huu ambao wataalamu wa mambo
wanadai kuwa ni kama jibu kwa Mhe Makonda.
MAKONDA AZIJIBU TUHUMA ZA KUTOKA NA MASOGANGE KIAINA AINA
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda ametupa jiwe gizani kwa
kumjibu Wema Sepetu baada ya siku chache zilizopita kuenea kwa sauti
yake mitandaoni akiwa mahabusu huku akimlalamikia mkuu huyo wa mkoa
kushindwa kulitaja jina la Agness Masogange kwenye orodha ya kwanza ya
watuhumiwa wa madawa ya kulevya.
KUMBE UWOYA ANAPENDA WANAUME WENYE SURA MBAYA
STAR wa Bongo Movie mwenye mvuto wa pekee na mshiriki wa shindano la
Ijumaa la Figa Bomba, Irene Uwoya, amefunguka kupitia ukurasa wake wa
Instagram kuwa havutiwi na wanaume wenye muonekano mzuri na hujui ni kwa
nini
Aidha staa huyo amewahi kuripotiwa na vyombo vya habari kuwa anavutiwa
sana na wasanii wa Bongo
Subscribe to:
Posts (Atom)