Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda ametupa jiwe gizani kwa
kumjibu Wema Sepetu baada ya siku chache zilizopita kuenea kwa sauti
yake mitandaoni akiwa mahabusu huku akimlalamikia mkuu huyo wa mkoa
kushindwa kulitaja jina la Agness Masogange kwenye orodha ya kwanza ya
watuhumiwa wa madawa ya kulevya.
Akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari Jumatano hii ofisini kwake
wakati akitaja orodha ya pili ya watuhumiwa wa madawa hayo, Makonda
amesema, “Ukitaja jina kwanza utakuwa unaingia kama vile unajitahidi
kuhama.”
“Hebu wewe kama una taarifa za mitandao sahihi tuambie tu, ndio maana
nimesema tunapokea kwa wenyeviti wa mitaa, tunapokea wapi, wewe kama una
taarifa sahihi wewe tuambie tu. Lakini usiibue taarifa kwa sababu wewe
una jambo la kujibu ukaibua taarifa nyingine tena siyo rasmi, tena
nimeeleza hapa ukiwa kwenye mahabusu au popote pale chini ya usimamizi
hata simu huruhusiwi kuwa nayo,” ameongeza.
“Kwahiyo bado vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kucheki pia
utaratibu gani uliotumika kwa mtu kujirekodi na kuanza kutoa matangazo
wakati upo sehemu sahihi ya kutoa hizo taarifa.”
Majina 65 ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya yametajwa kwenye orodha ya
awamu ya pili yakiwemo majina makubwa nchini Freeman Aikaely Mbowe,
Yusuf Manji, Mchungaji Josephat Gwajima, Iddi Azan na Hussein Pambakali.
No comments:
Post a Comment