Friday 17 June 2016

TAARIFA YA KUZINGIRWA NYUMBA YA ASKOFU GWAJIMA, CHANZO HASA NI NINI? BOFYA HAPA

SUBSCRIBE HAPA
Taarifa ya kuzingirwa nyumba ya Askofu Gwajima, chanzo hasa ni nini? Bofya hapa
Watu sita wanaodhaniwa kuwa askari wa Jeshi la Polisi, wamevamia na kuizingira nyumba ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini, Josephat Gwajima.
Tukio hilo linadaiwa kutokea jana mchana katika makazi ya askofu huyo yaliyoko eneo la Salasala, Dar es Salaam.
Inadaiwa watu hao walifika nyumbani kwa askofu huyo wakiwa katika gari aina ya Toyota Land Cruiser, na kwenda kugonga geti ili wafunguliwe waingie ndani.
Picha mbalimbali zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii jana, ziliwaonyesha
watu hao wakiwa wameizingira nyumba hiyo, huku wakiwa wamebeba bunduki zao vifuani.
Kitendo cha kuzingirwa nyumba ya askofu huyo aliyejibatiza jina la ‘Mr Tanzania’, kilizusha hofu miongoni mwa waumini wa kanisa lake na kuibua mijadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
Kupitia ukurasa wa mtandao wa Facebook wa kanisa hilo, Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano, David Mgongolwa, alililazimika kulitolea ufafanuzi tukio hilo.
Mgongolwa aliandika: “Kuhusu kuzingirwa kwa nyumba ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Duniani, Dk. Josephat Gwajima mchana huu na watu wasiojulikana.
“Viongozi wa Juu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Duniani pamoja na mwanasheria wa kanisa wanafuatilia kwa karibu na tutatoa taarifa kamili hapo baadaye. Tunaomba watu wote tuwe watulivu.”

No comments:

Post a Comment

advertise here