Thursday, 5 January 2017
WAZIRI MKUU AONYA UJENZI HOLELA MANISPAA YA KIGAMBONI
WAZIRI
Mkuu, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Manispaa ya Kigamboni
kuhakikisha unasimamia ujenzi wa kisasa na kutenga maeneo maalumu ya
wazi katika manispaa hiyo, ili kuepusha makosa ya ujenzi holela
yaliyofanyika katika maeneo mengine jijini Dar es Salaam.
Pamoja
na hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amesema manispaa
hiyo mpya kwa sasa inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa majisafi na
salama na wakazi wake wanatumia maji ya visima pekee ambayo si safi na
salama.
SHERIA YA OBAMACARE TRUMP KUITUPILIA MBALI KWA KISHINDO
Rais Barack Obama amewahimiza
wanachama wa chama cha Democratic kupigania sheria yake ya bima ya afya
ambayo utawala wa Donald Trump umeahidi utaibatilisha upesi baada ya
kuingia madarakani.
Kwenye mkutano wa faraghani wa saa mbili, Bw
Obama aliwahimiza wabunge wa chama hicho kuitetea sheria hiyo, huku
wanachama wa Republican nao wakichukua hatua kufuta sheria hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)