Na Regina Mkonde
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam jumanne ya Machi 13, 2017 katika eneo la Mongo la Ndege, limeokota mwili wa mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Imelda Ngonyani (13) aliyekufa maji wakati akijaribu kuvuka mto Msimbazi.
Akizungumza na waandishi wa habari Machi 14, 2017, Kamishna wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro amesema marehemu huyo kabla ya kufa maji alikuwa pamoja na wenzake watano walionusurika kifo wakielekea shule ya Msingi ya Mongo la Ndege.