Monday, 1 May 2017

WEMA SEPETU JOKATE WAPIGWA STOP SWALA LA WANAUME


Mikakati ya kusaka nafasi ya kuingia bungeni mwaka 2020 kwa walimbwende wa Bongo, Wema Isaac Sepetu na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, imenoga baada ya mastaa hao kutakiwa kutengeneza sifa ‘CV’ nzuri kwa kupigwa ‘stop’ kuhusishwa na skendo za wanaume kama walivyozoeleka, Wikienda limedokezwa.

TUNDU LISSU AKOMALIA VYETI VYA BASHITE KOTINI


WAWKILI Tundu Lissu na wenzake wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamelikomalia vilivyo sakata maarufu la Bashite linalohusiana na tuhuma za kughushi vyeti vya kielimu linalomkabili mmoja wa wakuu wa mikoa kwa kulifikisha kortini ili lipatiwe ufumbuzi.
 
Aidha, Lissu na wenzake hao wamedhamiria kuona kuwa kigogo huyo anayetuhumiwa kuliacha jina lake halisi la Daudi Albert Bashite kutokana na matokeo mabovu ya sekondari na kutumia jina la mtu mwingine, achukuliwe hatua za kisheria ikiwamo kufungwa jela kwa kosa la kughushi ikiwa itathibitika kuwa ana hatia.

advertise here