Wednesday 2 November 2016

AINA TATU YA MAWAZO YANAYOZUIA USHINDWE KUFANIKIWAA

Kiasili binadamu tumepewa uwezo mkubwa wa kufikiri ukitofautisha na wanyama wengine. Uwezo huu tulionao huwa unakuja hasa kutokana na matumizi ya mawazo au kufikiri kwetu. Kufikiri huko ambapo tunafanya kila siku na kila wakati ndipo kunapotufanya tuwe na maisha ya aina fulani, haijalishi yawe ya mafanikio au kushindwa.

Lakini hata hivyo wengi wetu huwa tunafikiri au tuna mawazo ya kimazoea na kushindwa kutambua kwamba hayo mawazo yetu pia yamegawanyika. Kwa mawazo yoyote uliyonayo mara huwa yamegawanyika katika sehemu. Kwa mfano unapowaza wazo fulani, wazo hilo linakuwa lipo moja

KAZI: MAMBO YA MSINGI KUZINGATIA KABLA YA KUACHA KAZI

Leo hii karibu kila mtu aliyeajiriwa ukimuuliza je, unafurahia maisha ya kuajiriwa? Atakwambia hapana ila natamani kujiajiri, na endapo utaendelea kumuuliza ni kwa nini unatamani kujiajiri? Utamsikia anasema nataka kuwa huru na muda na pia nahitaji uhuru wa kipesa.

Majibu hayo kwa mtazamo wa wengi ni sawa, ila kuna kitu ambacho ni vyema ukakijua kabla ya kuamua kuacha kazi na kwenda kujiajiri.

Kujiajiri kuna hitaji ujasiri wa hali ya juu sana maana kuna changamoto zaidi ya kuajiriwa. Hivyo nakusihi  ufikirie kwa umakini sana suala zima la kuacha kazi kabla kwenda kujiajiri.

Na endapo utaamua kuacha kazi ya kuajiriwa bila ya kufikiria ipo siku utakuja kujutia uamuzi wako. Hivyo ni vyema ukafikiria mara mbili kabla ya kufanya maamuzi magumu.

Mambo ya msingi ya kuzingatia kabla ya kuacha kazi.

1. Kuwa na nidhamu ya muda.
Kwa kuwa kwa sasa bado umeajiriwa, hivyo huna jukumu la kufanya maamuzi ya matumizi ya muda, Bali unafanya kazi kutokana na muda ambao muajiri wako ameamua yeye kukupangia kuweza kufanya kazi.

Na kwa kuwa umezoea kufanya kazi kutokana na amri ya mwajiri wako, hata pale ambapo utaamua kuacha kazi fahamu fika ya kwamba suala la kuwa na nidhamu ya muda kwako ni suala gumu, hivyo unatakiwa kufanya jitihada zako binafsi kadri iwezekanavyo hasa katika matumizi sahihi ya kufanya kazi hasa suala zima la uzalishaji wa mali au huduma.

Nazungumza suala zima la matumizi ya muda kwani hapa ndipo ambapo tunapata makundi mawili ya watu waliofanikiwa na wasiofanikiwa. Hivyo ni jambo jema kuhakikisha unazingatia matumizi sahihi ya muda ili pindi utakapoacha kazi wewe ndiye ambaye utakuwa na jukumu la kupanga muda wa kufanya kazi na ni muda gani utakuwa ni wa kupumzika. Pia ikiwezekana ongeza matumizi sahihi ya muda mara mbili zaidi ya ulivyokuwa umeajiriwa.

2. Kutokuahirisha kufanya mambo ya msingi.
Utakuwa shahidi ya kwamba wakati umeajiriwa suala zima la uahirishaji wa kufanya mambo ya msingi lilikuwa ni suala gumu sana labda awe ameamua mwajiri wako. Kama ndivyo hivyo basi pale ambapo utakuwa umeamua mwenyewe kuacha kazi na kuamua kufanya kazi mwenyewe hivyo huna budi kuhakikisha ya kwamba suala zima la uhairishaji mambo linakuwa ni suala ambalo halina nafasi katika maisha yako.

Ukiwa ni mtu wa kufanya kazi kwa kuamua kutenda bila kuahiirisha vitu vya msingi ama hakika utafika kilele cha mafanikio yako ndani ya muda mfupi. Ni vyema kulizingatia hili, kwani hili ndilo ambalo limewafanya watu wengi ambao waliacha kazi kuwa na maisha duni zaidi, kwani wengi wao walikuwa ni waahirishaji wazuri wa vitu vya msingi

GABO KULIZIBA PENGO LA KANUMBA

Msanii wa filamu anayefanya vizuri na filamu ‘Safari ya Gwalu’ Salim Ahmed aka Gabo Zigamba amefunguka kwa kusema kuwa wasanii wa filamu wakiwa na juhudi wanaweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba.

Mwigizaji huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wa filamu ambao wanafanya vizuri kwa sasa, amedai kama wasanii wakiamua kufanya kazi kwa bidii basi kila kitu kinawezekana.

advertise here