Monday 6 April 2015

MALEGEND AMBAO NI WAJASILIAMALI WAKUBWA WA KUIGWA

NA SWAXBZ LAYIIIIIIIIII

Sean John ' P. Diddy'.
LICHA ya wasanii nyota wa filamu wa Hollywood nchini Marekani kuingiza fedha nyingi kutokana na kuigiza na kudhaminiwa na makampuni makubwa, waigizaji wa Nigeria waliochini ya Nollywood, mambo yao hayaendi vizuri kama wanavyotaka.
Pamoja na kupata mafanikio makubwa katika kuigiza, waigizaji wa Marekani wamejiingiza katika sanaa nyingine nyingi kama yale ya fasheni za mavazi ambako wameingiza mkwanja mkubwa.
Nyota ambao wanaingiza mkwanja mkubwa kila mwaka katika anga hizo, kwa mujibu wa gazeti la Forbes ni pamoja na Nicole Richie ambayo imemwingizia Dola milioni 2, Rachel Zoe Collection (milioni 20), Justin Timberlake na rafiki yake Trace Ayala (milioni 50), Gwen Stefani (milioni 90) na . Victoria Beckham milioni 95) alizovuna mnamo mwaka 2011 peke yake.

advertise here