Wednesday, 10 February 2016

AJALI MBAYA YATOKEA MANDELA ROAD DAR-ES-SALAAM

LAYIII


Habari zilizoenea kwa kiasi kikubwa kwa watumiaji wa barabara ya Mandela jijini Dar Es Salaam ni kuhusiana na ajali iliyotokea ya kontena kuangukia basi dogo la abiria maarufu kama daladala na gari ndogo. Ajali hiyo kwa taarifa za awali inatajwa kutokea maeneo ya Tabata. Kwa mujibu wa mtandao wako wa press bongo....... inafuatilia kwa kina taarifa kamili ili kukuletea habari za uhakika zaidi ila hizi ni picha za mwanzo kuhusu ajali hiyo

MJUE MKONGO POLICE AMBAYE NI MWANAMZIKI

LAYIII

Polisi ambaye ni mwanamuziki DR Congo

5 Februari 2016 Imebadilishwa mwisho saa 16:50 GMT
Kwa kawaida polisi huzingatiwa kuwa watu wenye kuwaandama wahalifu na kila wakati wanapoonekana, wengi hujiuliza kwani leo kulikoni?
Na hali huwa ni ya wasiwasi zaidi ikiwa mmoja wa maafisa hao wa polisi ni wa cheo cha juu.
Bahati Kasamba Innocent, ni afisa wa cheo cha juu ndani ya idara ya polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayesifika sana katika fani ya uimbaji wa nyimbo za Injili.
Anasema yeye huimba katika juhudi za kuhubiri amani, uongozi bora na pia upendo.
Mwandishi wa BBC Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Byobe Malenga huko Bukavu, alikutana na msanii huyo studioni akiandaa baadhi ya nyimbo zake.


UTAFITI UNAONYESHA KUWA FARASI HUTAMBUA HISIA ZA MWANADAMU.....

LAYIII



Farasi huweza kubaini kati ya mtu aliye na furaha na aliye kasirika kwa kuangalia uso wa mwanadumu,utafiti umesema.
Katika jaribio, kwa kutumia picha za mwanamume wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Sussex walionyesha kwamba farasi wanaofugwa nyumbani huchukizwa na sura zilizokasirika.
Wanasayansi hao wanasema kuwa ufugaji huo huenda umewawezesha farasi kuelewa tabia za binaadamu.

advertise here