5 Februari 2016 Imebadilishwa mwisho saa 16:50 GMT
Kwa
kawaida polisi huzingatiwa kuwa watu wenye kuwaandama wahalifu na kila
wakati wanapoonekana, wengi hujiuliza kwani leo kulikoni?
Na hali huwa ni ya wasiwasi zaidi ikiwa mmoja wa maafisa hao wa polisi ni wa cheo cha juu.
Bahati
Kasamba Innocent, ni afisa wa cheo cha juu ndani ya idara ya polisi
nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayesifika sana katika fani ya
uimbaji wa nyimbo za Injili.
Anasema yeye huimba katika juhudi za kuhubiri amani, uongozi bora na pia upendo.
Mwandishi
wa BBC Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Byobe Malenga
huko Bukavu, alikutana na msanii huyo studioni akiandaa baadhi ya nyimbo
zake.
No comments:
Post a Comment