Monday 3 April 2017

ALIYETUMBULIWA NA RAIS MAGUFULI DK MWELE MALECELA ATEULIWA KUWA MKURUGENZI SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO)..!!!


Salamu za pongezi zimeendelea kumiminika kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr), Dk Mwele Malecela baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika vya Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika.

Pia, Dk Mwele  aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mpango wa Maalumu wa WHO wa kutokomeza magonjwa yasiyopewa kipaumbele (Espen) na sasa atahamia kituo chake cha kazi Congo-Brazaville. 

Mradi wa Espen ulianza kutekelezwa mwaka 2016 hadi 2020, una lengo la kumaliza magonjwa yasiyopewa kipaumbele kwa kutoa vifaa tiba, elimu na dawa. 

advertise here