Hatimaye imedhibitika kuwa Mwenyekiti wa Timu ya soka ya Yanga na
Mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania Yusuph Manji anatumia madawa ya
kulevya na leo atapandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo akiwa pamoja na
watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kwa sakata kama hilo.
Katika Kipindi cha michezo katika redio moja nchini Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amethibitisha kuwa
vipimo vya Mkemia Mkuu wa Serikali alivyofanyiwa Manji
vinaonyesha kuwa ni Mtumiaji wa Madawa ya kulevya (Hakuyataja aina yake) na kusisitiza kuwa leo mtuhumiwa huyo atapandishiwa kizimbani kujibu shitaka hilo.
vinaonyesha kuwa ni Mtumiaji wa Madawa ya kulevya (Hakuyataja aina yake) na kusisitiza kuwa leo mtuhumiwa huyo atapandishiwa kizimbani kujibu shitaka hilo.
Akielezea afya yake tangu alazwe Hospitali, Kamanda Sirro amesema kuwa
mwenyekiti huyo wa yanga yuko vizuri na sasa ameruhusiwa kutoka
Hospitalini na kurejeshwa mahabusu polisi kusubiri kupandishwa
kizimbani.
Sirro amesema kuwa habari kamili kuhusu sakata hilo na watuhumiwa
wengine wakiwemo wasanii waliokamatwa zitatolewa leo mbele ya wanahabari
Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment