Shirikishio la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeishukuru kampuni
ya bia ya Heineken ambao ni wadhamini wakuu wa michuano ya Ligi ya
Mabingwa barani Ulaya (UEFA) kwa kujitolea kufanya ukarabati wa viwanja
vitatu vya mpira wa miguu vilivyopo jijini Dar es salaam.
Katika barua ya Meneja Mkuu wa Heineken nchini Tanzania, Michael
Mbugu kwenda kwa wakurugenzi ya Manispaa wilaya za Ilala na kinondoni,
nakala yake kutumwa kwa Rais wa TFF, imeeleza mdhamini ameelekeza nguvu
zake kwenye kukarabati baadhi ya viwanja nchini ili viwe katika hali
nzuri na salama ili kukuza vipaji vya vijana kwenye mchezo wa soka.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezitakia kila la
kheri klabu za Azam FC na Young Africans ambao ni wawakilishi pekee wa
Tanzania katika michuano ya kimataifa itayochezwa wikiendi hii.
TFF imevitaka vilabu hivyo kupambana katika michezo inayowakabili na
kuweza kufanya vizuri kwa kupata ushindi, ili kutengeneza mazingira
mazuri katika michezo ya marudaino itakayochezwa Aprili 19-20 mwaka huu.
Stori: Mayasa Mariwata na Gladness mallya, Ijumaa
Wakati mama yake, Flora Mtegoa (pichani), baadhi ya wasanii na mashabiki
wake wakikumbuka miaka minne ya kifo cha aliyekuwa staa mkubwa wa
filamu za Kibongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great’, kumezuka
sintofahamu ya kukutwa ujumbe mzito wa kimapenzi kaburini kwa msanii
huyo ambao unadaiwa kuwekwa na mrembo aliyefika mahali hapo mapema wiki
hii.