LAYIII
"IKULU SIO YA BABA'KO"!
Hii ni kauli ambayo inatumika kwenye Project Mpya ya kisiasa inayovuma nchini kwa jina la DJ (Dogo Jembe).
Projekti hii, yenye uwekezaji mkubwa na inayofanyika kwa viwango vya hali ya juu vya kiteknolojia katika uzalishaji na usambazaji wake, inamtumia kijana wa umri chini ya miaka 18, ambaye anataja mifano ya changamoto za nchi na kuzishangaa ni kwa namna gani zinashindwa kutatuliwa wakati inawezekana!
Kinachoipa nguvu hii projekti, ni namna ambavyo DJ huyo ameweza 'kuchukua' fomu ya Urais kupitia CCM na kutia nia ya kujitosa kwenye uongozi huo wa juu, ili kuweza kuwafundisha mafisadi cha kufanya katika kuiletea nchi maendeleo kwa upande wa afya, elimu, miundombinu na kadhalika.
Kwa namna inavyoendeshwa, hakuna shaka kwamba ina 'mkono mzito' wa mmoja wa watia nia ya urais nchini. Ni jambo jema, lakini usiri wake unazua maswali lukuki.
Watu wengi sasa wanajiuliza; Je, Ni nani aliye nyuma ya hii projekti? Ni nini haswa 'motive' ya hii projekti? Anafaidikaje kutokana na huu uwezekezaji?
Sasa basi, Napenda tusugue vichwa kwa pamoja, na tuanze kuunganisha nukta ili kuweza kumtambua muhusika wa hili suala.
Tuko nyakati za mambo mengi sasa kisiasa, kwahiyo ni vema tukajua michezo yote inayochezwa, iwe misafi ama michafu ili tusije tukaachwa feri!

Dondoo: Huu mradi
unamiliki tovuti ya kisasa, vipande vya video vimerekodiwa kwa ubora wa
hali ya juu, Kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii zimedhaminiwa, na
waandishi wa habari wenye wafuasi wengi pia wanashiriki kuisambaza
(mfano, MillardAyo).