Mkazi wa kitongoji cha Kazima – Kichangani Kata ya Kawajense,
Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Emmanuel Joseph (31) amemfanyia unyama
mtoto wake wa kumzaa, George Emmanuel (4) kwa kuvichoma kwa moto vidole
vyake vya mkono wa kushoto, akimtuhumu kukomba mboga yote ya majani
aina ya ‘chainizi’ yenye thamani ya Sh 500.
Inasemekana baba huyo amekuwa akiishi na watoto wake watatu baada ya
kuachana na mkewe wa ndoa, Semsni Jahala (28) Machi mwaka jana.