LAYIII
Mkazi wa kitongoji cha Kazima – Kichangani Kata ya Kawajense, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Emmanuel Joseph (31) amemfanyia unyama mtoto wake wa kumzaa, George Emmanuel (4) kwa kuvichoma kwa moto vidole vyake vya mkono wa kushoto, akimtuhumu kukomba mboga yote ya majani aina ya ‘chainizi’ yenye thamani ya Sh 500.
Inasemekana baba huyo amekuwa akiishi na watoto wake watatu baada ya kuachana na mkewe wa ndoa, Semsni Jahala (28) Machi mwaka jana.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Rashid Mohamed akiwa mjini Mpanda alithitibisha kuwa mkasa huo ulitokea juzi saa 12 jioni katika kitongoji cha Kazima– Kichangani.
Akisimulia mkasa huo, Kaimu Kamanda Mohamed alisema mtuhumiwa huyo amekamatwa kwa mahojiano na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali wa shauri lake kukamilika.
“Jioni hiyo ya tukio saa kumi na moja jioni mtuhumiwa huyo (Emmanuel) alipika chakula cha jioni, ugali na mboga za majani maarufu chainizi kisha akakihifadhi chakula hicho jikoni na kuondoka … aliporudi nyumbani saa kumi na mbili jioni ili kuandaa chakula cha jioni ndipo alipobaini mtoto wake (George) amekomba mboga yote ya majani. Alikasirishwa na kitendo hicho na kusababisha kumpiga kisha kumchoma moto vidole vyake vitatu vya mkono wa kushoto na kumsababishia maumivu makali,” alieleza Kaimu Kamanda.
CHUKUA MUDA WAKO KUONA JINSI DUNIA INAVYOKWENDA NA WALIMWENGU WANAVYO FANYA Kwa mujibu wa mashuhuda kutoka eneo hilo la tukio, mtoto huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambako amelazwa kwa matibabu.
Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda, Oscar Mkenda alisema mke aliamua kuachana na mumewe huyo baada ya kuchoshwa na ukatili na unyanyasaji aliokuwa akifanyiwa, ikiwemo kupigwa mara kwa mara bila ya sababu yoyote.
“Mtoto George alikomba mboga hizo zote za majani baada ya kushinda na njaa mchana kutwa kwani hata kifungua kinywa hakupa asubuhi… hivyo baada ya baba yake kubaini mtoto wake George amekomba mboga zote, ndipo alipochochea moto na kuukandamiza mkono wake wa kushoto na kuunguza vibaya vidole vyake vitatu,” alieleza Mkenda.
Muuguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda, Joseph Mkangwa alieleza kuwa mtoto George amelazwa katika wadi namba nne kwa matibabu na kwamba hali yake bado ni tete. Mtoto huyo anatunzwa hospitalini hapo na nyanya yake, Hadija Ally.
Chanzo: Habari Leo.

No comments:
Post a Comment