Thursday, 15 January 2015

DIAMOND ADHIBITISHA KUWA ZARI ANA MIMBA YAKE

MWANAMKE MWENYE KOVU JEUSI

HEKA HEKA MJINI NI HADITHI NZURI YA KUSISIMUA NA KU VUTIA
Nakumbuka vizuri ilikuwa siku ya jumapili ambayo kama ilivyoada kwangu huwa sikosi kwenda kanisani hasa misa ya kwanza kwani huwa napenda sana kusali misa ya kwanza ili baadaye niweze kuendelea na mambo yangu mengine,siku hiyo niliamka asubuhi na mapema kutoka pale nyumbani kwangu mnazi mmoja karibia na ofisi za chama cha mapinduzi za mkoa wa Dar-es-salaam na kuelekea kanisani pale saint.alban posta taratibu kwa miguu kwani gari yangu ilikuwa imeharibika wiki ya pili sasa na isitoshe pale nyumbani kwangu mpaka pale posta hapakuwa mbali sana kiasi cha kama dakika 20 tu hasa kwa kijana kama mimi ambaye damu ilikuwa bado inachemka.niliingia pale kanisani nikiwa sijachelewa sana misa ilikuwa imeanza kama dakika 7 hivi nakumbuka sana somo la siku hiyo alilolitoa padri Kiaka lilikuwa linahusu umuhimu wa kuombea siku yako ya kufa kwani haina siku wala saa.

Mahakama yasitisha mgomo wa walimu Kenya

Mgomo wa walimu wa shule za umma nchini Kenya umesitishwa baada ya agizo la mahakama kwamba walimu warejee kazini wiki ijayo ikiwa afueni kwa wanafunzi
Agizo hilo limetolewa baada ya mazungumzo ya siku nzima kati ya chama cha kutetea masilahi ya walimu pamoja na upande wa serikali katika mahakama ya viwanda.
Mahakama hio imewaaamuru walimu kurejea kazini na kwamba hakuna anayepaswa kuchukulia hatua za aina yoyote kwani mgomo huo ulikuwa halali.
Serikali pamoja na upande wa walimu zimetakikana kuwasilisha mapendekezo kuhusiana na malipo ambayo walimu wanataka.
Mazungumzo hayo, yananuiwa kusuluhisha mgogoro wa malipo kati ya walimu na serikali.
Kufuatia agizo hilo la mahakama , walimu wanatarajiwa kurejea kazini Jumatatu huku wazazi na wanafunzi wakipata afueni.
Juhudi za hapo awali kujaribu kuzuia mgomo huo hazikufua dafu huku mgomo huo ukiingia katika wiki yake ya pili.
Wabunge pia waliitaka serikali kusuluhisha mgomo huo na kuwapa walimu wanachotaka kwani wanafunzi hawajafunza tangu muhula mpya wa shule kuanza nchini Kenya.


advertise here