Thursday, 15 January 2015

Mahakama yasitisha mgomo wa walimu Kenya

Mgomo wa walimu wa shule za umma nchini Kenya umesitishwa baada ya agizo la mahakama kwamba walimu warejee kazini wiki ijayo ikiwa afueni kwa wanafunzi
Agizo hilo limetolewa baada ya mazungumzo ya siku nzima kati ya chama cha kutetea masilahi ya walimu pamoja na upande wa serikali katika mahakama ya viwanda.
Mahakama hio imewaaamuru walimu kurejea kazini na kwamba hakuna anayepaswa kuchukulia hatua za aina yoyote kwani mgomo huo ulikuwa halali.
Serikali pamoja na upande wa walimu zimetakikana kuwasilisha mapendekezo kuhusiana na malipo ambayo walimu wanataka.
Mazungumzo hayo, yananuiwa kusuluhisha mgogoro wa malipo kati ya walimu na serikali.
Kufuatia agizo hilo la mahakama , walimu wanatarajiwa kurejea kazini Jumatatu huku wazazi na wanafunzi wakipata afueni.
Juhudi za hapo awali kujaribu kuzuia mgomo huo hazikufua dafu huku mgomo huo ukiingia katika wiki yake ya pili.
Wabunge pia waliitaka serikali kusuluhisha mgomo huo na kuwapa walimu wanachotaka kwani wanafunzi hawajafunza tangu muhula mpya wa shule kuanza nchini Kenya.


No comments:

Post a Comment

advertise here