HEKA HEKA MJINI NI HADITHI NZURI YA KUSISIMUA NA KU VUTIA
Nakumbuka vizuri
ilikuwa siku ya jumapili ambayo kama ilivyoada kwangu huwa sikosi kwenda
kanisani hasa misa ya kwanza kwani huwa napenda sana kusali misa ya kwanza ili
baadaye niweze kuendelea na mambo yangu mengine,siku hiyo niliamka asubuhi na
mapema kutoka pale nyumbani kwangu mnazi mmoja karibia na ofisi za chama cha
mapinduzi za mkoa wa Dar-es-salaam na kuelekea kanisani pale saint.alban posta
taratibu kwa miguu kwani gari yangu ilikuwa imeharibika wiki ya pili sasa na
isitoshe pale nyumbani kwangu mpaka pale posta hapakuwa mbali sana kiasi cha
kama dakika 20 tu hasa kwa kijana kama mimi ambaye damu ilikuwa bado
inachemka.niliingia pale kanisani nikiwa sijachelewa sana misa ilikuwa imeanza
kama dakika 7 hivi nakumbuka sana somo la siku hiyo alilolitoa padri Kiaka
lilikuwa linahusu umuhimu wa kuombea siku yako ya kufa kwani haina siku wala
saa.
Misa ilipoisha mida ya
saa 3 asubuhi niliona nijivute mpaka mitaa ya upanga pale nyuma ya diamond
jubilee mwendo wa pole pole nikamuone
rafiki yangu Martin ambaye pia alikuwa ni mfanyakazi mwenzangu. Sikutaka
hata kumtaarifu kwenye simu kwani simu yangu haikuwa na pesa pia nilijua kwa
kuwa tuliahidiana jana kwamba kesho nikitoka kanisani nitaenda kwake basi haina
shaka nitamkuta tu kwani pia Martin huwa sio mzururaji sana hasa mida ya
asubuhi kama haendi kazini.Wakati naingia ndani kwa rafiki yangu kipenzi Martin nakumbuka ilikuwa ni mida ya saa 4 asubuhi
mlangoni nilipishana na mdada wa makamo mweusi kiasi ambaye nakumbuka vizuri
alikuwa amevalia dela la rangi ya kijani kibichi likiwa linamichirizi ya rangi
ya zambarau na kwa ndani alikuwa amevaa suruali ya jeans ya rangi nyeusi huku kichwani akiwa amejifunga mtandio
mweusi kufunika nywele zake nilimsalimia aliitikia haraka haraka huku
akikwepesha sura yake na huku akionyesha ni mtu aliyekuwa na shauku ya kuondoka
lile eneo haraka sana, mimi hata sikumjali nilijua atakuwa ni mmoja kati ya
wasichana ambao alikuwa na uhusiano nao bwana Martin kwa kuwa rafiki yangu
Martin alikuwa ni mtu aliyependa sana wasichana,nilifika mpaka pale alipokuwa
amepanga Martin ilikuwa ni nyumba ya uwani akiwa amepanga chumba na sebule huku
nyumba ya mbele kukiwa hakuna mtu hata mmoja aliyekuwa amepanga kwa maelezo
yake ile nyumba ya mbele kulikuwa na mpangaji lakini amehama na sasa mwenye
nyumba alikuwa yupo akiifanyia marekebisho tayari kwa kuingia mpangaji
mwingine. Ile nimefika tu mlangoni nikakuta mlango upo wazi kitu ambacho
kikawaida sio busara kuingia nyumba ya mtu bila kugonga basi nikajivuta pale
mlangoni na kuanza kuugonga ule mlango hallow Martin hallow niligonga kama dakika tano bila kupata jibu
lolote kutoka mule ndani ilinibidi nishangae kidogo kwa maana hata kama
angekuwa msalani ni lazima angesikia ile sauti yangu na kwa nini akae kimya
sikuamini kama alikuwa amelala wakati nimepishana na Yule dada anatoka chumbani
kwake muda si mrefu,ikanibidi niingie tu ndani kama hayupo atanikuta mule mule
nikimsubili, mungu wangu sikuamini nilipoingia pale sebuleni kwake nilikutana
na michirizi ya damu kutoka pale sebuleni kuelekea chumbani kwake mh ikanibidi
nipitilize haraka moja kwa moja kule chumbani kwake ile kuingia tu nikakutana
na mwili wa Martin akinikodelea macho huku ukiwa umekakamaa huku pia ukiwa umegandana na damu na alama kubwa ya kisu
kwenye shingo yake,nilimkimbila pale alipokuwa amelazwa na kumuangalia mungu
wangu alikuwa tayari ameshakufa,nilifikiria pale haraka haraka ni kipi nifanye
nikaanza kuitafuta simu yake mule ndani mpaka nikaipata nikawapigia simu polisi
na kuwaeleza lile tukio sikutaka nijihusishe moja kwa moja na lile tukio ndio
maana niliamua kutumia simu yake pia simu yangu nilikuwa bado sijaweka vocha
kisha nikaanza kutoka nje kabla sijatoka nje ya chumba chake macho yangu
yakatua kwenye meza ndogo iliyokuwa mule chumbani kwake mara nikakutana na
karatasi imeandikwa kwa Wino Mwekundu
“NILIYEMUUWA NI MIMI MWANAMKE MWENYE KOVU
JEUSI” shiti moyo ulijikuta unasisimuka na kuanza kudunda dunda kwani lile jina
si mara ya kwanza kwangu kukutana nalo hasa kwenye kazi zangu,mungu wangu huyu
mwanamke amemuuwa tena na Martin? Martini amemfanyaje tena huyu mwanamke hatari
kama amemuuwa na Martin basi na mimi siku zangu haziko mbali hapana inabidi
nimzibiti kwa kila hali nilijikuta nimekaa naangalia ile karatasi aliyoandika
huku nikiutazama na mwili wake pale chini kwa muda wa dakika kadhaa mpaka
machozi yakaanza kunitiririka kwa mbali,nilishitushwa na kelele zilizotoka nje
nikahisi polisi watakuwa tayari wameshafika pale basi nikaona haina haja ya
kuondoka tena nikachukuwa shuka pale na
kuanza kuufunika ule mwili hallow inspector vipi tayari umeshafika? Habari
umeipataje? Ilikuwa ni sauti ya bwana Gerald mmoja wa ma afisa upelelezi pale
makao makuu, ndio mimi niliyewapigia simu nilimjibu kwa mkato huku nikimsaidia
kutoa vifaa vya kuchukulia finger print pamoja na camera digital ya kipelelezi
kupiga picha mule chumbani kwa ajili ya kupata nyayo zake na alama zingine za
Yule muuwaji,mkuu wangu wa kazi pia inspector Thomas na yeye pia alikuwa ni
mmoja ya watu waliokuwa wamefika pale kwa ajili ya kushuhudia lile tukio wakati
kina inspector Gerald wakiendelea kukusanya baadhi ya kumbukumbu mule ndani
bosi wangu aliniita nje alipiga simu hospitali ya taifa ya muhimbili
kuwajulisha kuhusu lile tukio kisha akaanza kuniuliza maswali kadhaa kuhusu
lile tukio aliniuliza kwanza nilijuaje kama Martin amekutwa na lile tukio
nikamjibu mimi mwenyewe imetokea tu kama bahati kwani tulikuwa tumepanga
kukutana naye siku ya leo nikitoka kanisani ili tuelekee bagamoyo kusherekea
siku ya mchumba wake ya kuzaliwa,ndio na mbona hili tukio tumejulishwa kupitia
simu yake aliendelea kunihoji, ni mimi ndiyo nilitumia simu yake kuwajulisha
kwani simu yangu haina pesa kabisa, je huyo muuwaji unamjua au unaweza kuwa
unamhisi nani? Ni MWANAMKE MWENYE KOVU JEUSI bosi wangu alijikuta anashituka
ohh wewe umejuaje? Aliniuliza kwa shauku kubwa ya kutaka kujua nimefahamu vipi
aliyefanya lile tukio ni mwanamke mwenye kovu jeusi nikamwambia kuwa kama kawaida
yake ameacha note juu ya meza mule chumbani mwa Martin ameandika kwa wino
mwekundu, basi bosi wangu alinituma nikamletee ile karatasi aliyoiacha huyo
mwanamke mwenye kovu jeusi,basi nilienda na kutoka nayo pale nje na kumpa
aiangalie, aliiangalia kwa muda wa kama dakika 2 hivi halafu akaludisha macho
kwangu na mimi muda ule nilikuwa pia nimemetolea macho basi tukajikuta
tumetoleana wote macho,hivi hakuna anayemjua huyu muuwaji? Kwa maana sasahivi
amezidisha haya mauaji alianzisha tena mazungumzo,
simjui ila uwezo wa kumpata
upo kwa nini asipatikane kwa maana tukimchekea tutajikuta na sisi wote
anatuondoa wakati nazunguma haya tayari gari ya kubebea wagonjwa kutoka
muhimbili hospitali ilikuwa tayari imeshafika pale nyumbani kwa marehemu Martin
tayari kwa kuchukua ule mwili kuupeleka hospitali ili ufanyiwe pia uchunguzi
mwingine wa kitabibu .Wale manesi walishuka kutoka ndani ya ya ile gari ya
kubebea wagonjwa na kuingia mule ndani tayari kwa kuuchukuwa ule mwili kwa
ajili ya kuupeleka hospitali.
******* ******************************
NINI KITAENDELEA FUATILIA KISA HIKI KWA UMAKINI
No comments:
Post a Comment