Tuesday 17 May 2016

Chelsea na Tottenham wapigwa faini kubwa

LIKE PAGE YETU HAPA 

Chelsea na Tottenham wamepigwa faini kutokana na mashtaka matatu ya kushindwa kuwadhibiti wachezaji wao katika sare ya 2-2 katika uwanja wa Stamford Bridge.
Chelsea watalazimika kulipa pauni 375,000 baada ya kukiuka sheria za shirikisho la soka nchini Uingereza kuhusu makabiliano ya wengi ikiwa ni mara ya nne tangu mwezi Novemba 2014.
Spurs wamepigwa faini ya pauni 225,000 ikiwa ni kisa chao cha tatu kutokea.Mechi hiyo ilikuwa na kadi 12 za manjano .
Mapema mwezi huu mchezaji wa Spurs Mousa Dembele alipigwa marufuku kwa mechi sita kutokana na ghasia katika mechi hiyo hiyo ambayo ambayo ilimaliza matumaini ya Tottenham kushinda ligi ya Uingereza.
Kiungo wa kati wa Ubelgiji Dembele mwenye umri wa miaka 28 alionekana akimgusa jicho

POLICE KENYA WASHUTUMIWA KWA UKATILI

LIKE PAGE YETU HAPA FACEBOOK
Polisi
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu nchini Kenya yameshutumu maafisa wa polisi wakisema walitumia nguvu kupita kiasi kukabili waandamanaji jijini Nairobi Jumatatu.
Tume ya Taifa ya Haki za Kibinadamu (KNHRC) imesema imeshangaza sana na video na picha ambazo zinaenea kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuhusu yaliyojiri wakati wa maandamano hayo.

advertise here