Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete amefunguka kuhusu madai ya baadhi ya watu kuwa ana utajiri wa kutisha na kwamba anamiliki mali nyingi, jambo ambalo limekuwa likifanya watu hao watilie shaka njia aliyotumia kupata utajiri huo.
Kikwete amesema kuwa anashangazwa na dhana hiyo potofu inayojengwa na watu bila kujua ukweli wa mambo, ambapo ameweka wazi kuwa yeye ni kijana mpiganaji na mwenye kupenda mafanikio,