Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezitakia kila la
kheri klabu za Azam FC na Young Africans ambao ni wawakilishi pekee wa
Tanzania katika michuano ya kimataifa itayochezwa wikiendi hii.
TFF imevitaka vilabu hivyo kupambana katika michezo inayowakabili na
kuweza kufanya vizuri kwa kupata ushindi, ili kutengeneza mazingira
mazuri katika michezo ya marudaino itakayochezwa Aprili 19-20 mwaka huu.
Young Africans wanaochezwa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa
barani Afria (CAF CL) watashuka dimbani kesho Jumamosi uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki, kucheza
dhidi ya Al Ahly katika mchezo namba 89 wa Ligi ya Mabingwa barani
Afrika (CAF CL).
Mchezo huo utachezeshwa na Dennis Dembele, akisaidiwa na Marius
Donatien, Moussa Bayere, mwamuzi wa akiba Tangba Kambou wote kutoka
nchini Ivory Coast, huku kamisaa wa mchezo huo akiwa Celestin
Ntangungira kutoka nchini Rwanda.
Jumapili katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi saa 9 kamili
alasiri, Azam FC watwakua wenyeji wa Esperance Sportive de Tunis (EST)
ya Tunisa katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC)
hatua ya 16 bora.
Waamuzi wa mchezo huo namba 75 ni Daniel Frazer Bennet, akisaidiwa na
Zakhele Siwela, Thembisile Theophilus, mwamuzi wa akiba Mbongiseni
Fakudze wote kutoka nchini Afrika Kusini, huku kamisaa wa mchezo akiwani
Joseph Nkole kutoka nchini Zambia.
No comments:
Post a Comment