Saturday 18 June 2016

INAONEKANA KUNA TATIZO KATI YA PRODUCER NAHREEL NA KUNDI LA WEUSI KUNA CHANZO KIONE HAPA

SUBSCRIBE HAPA MTU WANGU
https://www.youtube.com/watch?v=XW8wPiVJxpEHivi karibuni kumeibuka taarifa kuwa ule ukaribu uliokuwepo mwanzo kati ya kundi la Navy Kenzo na Weusi umepotea tangu yalipofanyika mabadiliko ya studio ya The Industry. Nahreel amesema hilo siyo kweli bado ni washkaji kama zamani tofauti watu wanavyowachukulia.

Navy Kenzo na Weusi wamekuwa watu wa karibu sana hali iliyopelekea watu kuona wivu kwa kusema kuwa Nahreel anawapendelea wasanii hao kwa kuwatengenezea beat nzuri zaidi ya wasanii wengine.

Akiongea na Bongo5, Nahreel amesema kuwa wao na Weusi bado ni washkaji na bado wana kazi zao kwenye studio yake hazijatoka.

“Ni kweli utaratibu umebadilika na mimi kama mfanyabiashara mwingine lazima kila siku niendelee kuweka
utaratibu fulani,” alisema Nahreel.

“Hapa kati nimekuwa busy na ratiba zangu na focus na Navy Kenzo tumekuwa tuna move hapa na pale kwahiyo unajua Weusi na wao wana mipango yao kama wana muziki siwezi nikawa mimi tu nawacheleweshea time zao, na hapa wana nyimbo nyingi zipo bado hazijatoka,” aliongeza.
CHUKUA MUDA WAKO KUONA VIDEO HII KIDOGO MTU WANGU

Hata hivyo Mei 6 mwaka huu Navy Kenzo walifanya sherehe za kuzindua studio yao ‘The Industry lakini hakuna hata msanii mmoja wa kundi la Weusi aliyehudhuria sherehe hizo.

Chanzo:Bongo5

No comments:

Post a Comment

advertise here