Wednesday 8 February 2017

USHAIDI DHIDI YA KESI YA SCOPIONI MAPYA YAIBUKA DAKTARI AIBUA USHAIDI MZITO


Shahidi wa nne katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njwete, ameieleza Mahakama kuwa mtu aliyehusika kumtoa macho Said Mrisho alikuwa ni mzoefu wa vitendo hivyo  na siyo wa kawaida.

Shahidi huyo, Dk Christine Mataka (52) ambaye ni daktari  bingwa  wa macho kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alitoa maelezo hayo katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala alipotoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa Njwete (34) katika kesi iliyopata umaarufu wa ‘kesi ya Scorpion’ kutokana na maelezo kwamba aliyefanya uhalifu huo ni Scorpion.

Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga, Dk Mataka kutoka kitengo cha macho alidai ilikuwa mara yake ya kwanza kuona mgonjwa aliyepelekwa Muhimbili akiwa hana vipande vya gololi za macho yote mawili.

Dk Mataka alidai mlalamikaji Said aling’olewa macho kwa kutumia kitu kikali kilichojikunja mbele ambacho kinaweza kutoa mboni ya jicho nzima bila kubaki kitu chochote.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule alidai kwa kawaida wagonjwa wanaopasuka jicho huwa wanakuwa na mabaki  au vipande vya gololi ya macho.

No comments:

Post a Comment

advertise here