Wednesday, 8 February 2017

VIDEO MAJIBU YA YUSUPH MANJI BAADA YA KUHUSISHWA NA MADAWA YA KULEVYA

Mfanyabiashara Yusufu Manji amesema kuwa atakwenda Kituo cha Polisi kesho kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivyotaka.
https://youtu.be/4lddMaRaAD4
Manji amesema kuwa pamoja na kuwa Makonda ametaka wafike Ijumaa yeye atakwenda kesho huku akihoji kuwa inawezekanaje wakaitwa watu 65 kuhojiwa kama hakuna shughuli za kufanya kwa siku nzima.
“Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa. Huwezi kunitangaza kupitia radio
kwamba niende kwenye kituo cha polisi saa tano. Makonda ni mdogo kwangu kiumri,” alisema mwenyekiti huyo wa Yangu akizungumza na waandishi mchana wa leo.
Amesema atakwenda polisi lakini pia hilo suala halitaisha hivyohivyo kwani atakwenda naye hadi mwisho.

No comments:

Post a Comment

advertise here