Wakati wasanii 13 wakipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu kwa nyakati tofauti na kuweka chini ya uangalizi, wenzao
wawili, Wema Sepetu na Omari Micheri wameendelea kusota rumande kwa
zaidi ya saa 120.
Wema na Omari ndiyo pekee katika kundi la wasanii waliojisalimisha
katika Kituo Kikuu cha Polisi tangu
Ijumaa iliyopita kwa tuhuma za ama kutumia au kuuza dawa za kulevya waliodaiwa kukutwa na vielelezo.
Ijumaa iliyopita kwa tuhuma za ama kutumia au kuuza dawa za kulevya waliodaiwa kukutwa na vielelezo.
Wakati Wema akidaiwa kukutwa na misokoto ya bangi, Omari anadaiwa
kukamatwa na kete nne za dawa za kulevya ambazo hazijafahamika.
SWAXBZ ONLINE SHOW COMING SUBSCRIBE YOUTUBE USIPITWE NA LOLOTE MTU WANGU
Juzi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro
alisema wasanii hao wangepelekwa mahakamani juzi pamoja na wenzao,
lakini wawili hao hawakupelekwa hadi jana.
Baada ya kufikishwa mahakamani, wasanii watano kati ya 13 waliwekwa
chini ya uangalizi wa mahakama kwa miaka mitatu huku wenzao wanane
wakiwekwa chini ya uangalizi wa mahakama wa mwaka mmoja.
Waliowekwa chini ya uangalizi wa miaka mitatu na Hakimu Mfawidhi,
Cyprian Mkeha na kutakiwa kuripoti polisi mara mbili kwa mwezi ni Ahmed
Hashim maarufu kama Petitman, Said Masoud Linnah maarufu kama Said
Alteza, Nassoro Mohamed Nassoro, Bakar Mohamed Khelee na Lulu Abbas
Chelangwa maarufu kama Luludiva.
No comments:
Post a Comment