Tuesday, 14 February 2017

MAAJABU: MIMBA MIEZI 13 AJIFUNGUA CHUA NA MDUDU MWENYE MANYOA MEUSI


Na Ibrahim Yassin, Kyela
MKAZI wa Kitongoji cha Njisi, Kijijiji cha Kilwa, wilayani Kyela, Tummanye Makula (35) , amekaa na ujauzito miezi 13 na kushindwa kujifungua.

Hata hivyo, baada ya maombezi, alijikuta akijifungua chura na baadaye mdudu wa ajabu akiwa na manyoya meusi.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki baada ya dada huyo kumpigia simu Mchungaji wa Kanisa la Tample Of Prayer For All Nations Church, Nabii Charles Mkuvasa wa mjini Kyela  akihitaji kuombewa.
Alicuhukua hatua hiyo  baada ya kukaa na ujauzito kwa muda wote huo na kushindwa kujifungua, licha ya
kuzunguka kwa waganga wa kienyeji.
Akizungumza na MTANZANIA  jana, Tummanye alisema aliachana na mume wake muda mrefu na kuamua  kuishi na mama yake mzazi.
Alisema baada ya miaka miwili, alipata mwanaume mwingine ambaye alimpa ujauzito huo na siku zote alikuwa akihudhuria kliniki katika Hospitali ya Wilaya Kyela.
Alisema ilipofika miezi tisa, alipata uchungu siku mbili, lakini hakujifungua  huku madaktari wakimweleza kuwa njia yake ni ndogo, licha ya kuwahi kuzaa mtoto mmoja.
Baada ya siku mbili uchungu huo   ulikata na aliendelea kukaa na ujauzito wake  hadi alipoamua kunywa dawa na kupiga lamri kwa waganga wa kienyeji, ingawa pia  hakufanikiwa lolote, alisema.
Alisema alipokuwa nyumbani aliambiwa na marafiki zake aende kwa Nabii Charles akaombewe kutokana na kutokuwa na uwezo wa kutembea na yeye aliomba namba ya simu na kumpigia.
Alisema Charles alianza kumuombea na baada ya dakika tano, alisikia uchungu ikabidi aingie ndani…muda mfupi alijifungua chura ambaye alitoweka katika mazingira ya utata.
“Nilitoka sebuleni na kumweleza mchungaji na mama yaangu nimejifungua chura ambaye ametoweka katika mazingira ya utatanishi,” alisema.
Alisema baada ya muda mfupi, alijisikia uchungu tena na kwenda chumbani na kujikuta akijifungua mdudu wa ajabu akiwa na manyoya kama paka na nywele za rasta, ikabidi amwite mama yake na mchungaji.
Mama mzazi wa Tummanye Makula  hakuweza kutaja jina wala kusema chochote, baada ya gazeti hili kufika  nyumbani kwake, isipokuwa alikuwa  akilia tu muda wote.
Mkazi wa Kyela, Bonifas Mwalila, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alisema tukio hilo ni la kwanza kuliona  tangu  azaliwe.
Naye Mchungaji Mkuvasa, alisema baada ya kufika kijijini alimkuta mama huyo akiwa katika hali mbaya, kifo kilikuwa kinamwita lakini kutokana na maombi alimnusuru.
Diwani wa Kata hiyo, Anna Makula licha ya kukiri kuwapo tukio hilo, alisema amekuwa akishuhudia matukio mengi ya watu kufika kanisani hapo wakiwa wamefungwa kamba, lakini baada ya siku tatu alikuwa akishangaa wakirudi makwao wakiwa wazima.
Chanzo:Mtanzania

No comments:

Post a Comment

advertise here