Waziri huyo mkuu mstaafu ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa ametoa rai hiyo kwa vijana wakati wa ufunguzi wa mkutanao mkuu wa kamati tendaji ya BAVICHA Taifa na ambapo amehimiza umoja ndani ya baraza hilo na kuwataka kuelekeza nguvu zao mwaka 2020, huku pia akiendelea kusikitishwa na kauli tata za katazo la mikutano ya kisiasa.
John Mrema na Bw. Patrobas Katambi ambaye ni mwenyekiti wa baraza hilo pamoja na masuala mengine wamewataka vijana kuwa mstari wa mbele kuhakikisha demokrasia inapatikana huku pia adhima yao ya kuelekea mjini dodoma wakisema iko pale pale.
Kikao hicho cha kamati kuu tendaji ya BAVICHA Taifa kilihudhuliwa na wajumbe kutoka mikoa yote Tanzania ambapo pia kinaratajia kutoka na azimio la njia mbadala ya kile inachokiita ni kwenda kulisaidia jeshi la polisi mkoani Dodoma.
VIDEO MAKONDA ALIVYOMSHTAKI MTU KWA RAIS MAGUFULI
No comments:
Post a Comment