LAYIII
Kilichotokea Bungeni mpaka Bunge likaahirishwa leo July 02 2015
Kikao cha Bunge kilianza kama kawaida
leo July 02 2015, baada ya kipindi cha maswali na majibu yaliyoulizwa
kwa Mawaziri, Mbunge John Mnyika akaomba mwongozo.
“Tumekabidhiwa
orodha ya shughuli za leo.. kimsingi imekiuka kanuni, uamuzi wa kuileta
hii miswada mitatu kwa pamoja kama hati ya dharura umekiuka kabisa
msingi wa makubaliano ya kwenye Semina ambapo Wabunge kwa kauli moja
tulikataa Miswada hii isiletwe kwa hati ya dharura“
“Naomba Mwongozo, hili jambo linahitaji majibu sasa” >>> Mbunge John Mnyika.
Spika Makinda akaanza kutoa ufafanuzi kuhusu hiyo ishu >>> “Toa kwanza maneno ya kuniamrisha mimi cha kufanya… Hakuna mtu anayeweza kuniamrisha” >>> Anne Makinda.
No comments:
Post a Comment